
Kimbunga kikali kinachoitwa Fung-wong kinatazamiwa kutua Ufilipino siku chache baada ya kimbunga Kalmagei kilichowaua zaidi ya watu 200. Fung-wong, kinatarajiwa kuambatana na upepo mkali na mvua kubwa katika maeneo mengi ya Ufilipino.
Shule, ofisi zafungwa kunusuru maisha ya watu
Shule na ofisi za serikali zimeamriwa kufungwa Jumatatu katika mji mkuu Manila ambako pia safari zaidi ya 300 za ndege zimefutwa.
Wanasayansi wameonya kuwa, vimbunga vinavyotokea sasa vinazidi kuwa na nguvu zaidi kutokana na athari za mabadiliko ya tabianchi zinazosababishwa na binadamu.