Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kimeeleza kuwa Jeshi la Polisi limewaachilia kwa dhamana viongozi wake wanne, akiwemo Makamu Mwenyekiti Bara, John Heche, Naibu Katibu Mkuu Bara, Amani Golugwa, Mjumbe wa Kamati Kuu, Godbless Lema na Mwenyekiti wa CHADEMA Kanda ya Pwani, Boniface Jacob.
Jioni ya leo, viongozi hao wameonekana wakitoka kwenye Kituo cha Polisi cha Oysterbay jijini Dar es Salaam.
#AzamTVUpdates
Mhariri | John Mbalamwezi