Elimu ya ufundi inayotolewa na vyuo vya umma vya maendeleo ya wananchi (FDC) imeonekana kuwa mkombozi kwa vijana wengi waliokosa fursa za elimu kutokana na sababu mbalimbali, ikiwemo umasikini.

Katika tawi la FDC Malampaka, wilayani Maswa, baadhi ya vijana akiwemo Faustine Edward wamesema mafunzo ya ufundi waliyopata yamewasaidia kuepuka makundi maovu na kujiajiri kwa kutumia fursa za nishati ya umeme na ujenzi wa Reli ya SGR.

#AzamTVUpdates
Mhariri | John Mbalamwezi

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *