#HABARI: Mbunge Mteule wa Ilala, Mussa Azzan Zungu, ameibuka mshindi wa nafasi ya Spika wa Bunge la 13 la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania baada ya kupata kura 378 kati ya wagombea watano.

Matokeo yametangazwa Novemba 11, 2025, ambapo wapinzani wake hawakufikia kura mbili kila mmoja.

Zungu, ambaye amehudumu Bungeni tangu 2005, amewahi kuwa Mwenyekiti wa Bunge (2012–2021) na Naibu Spika (2022–2025). Ana elimu ya Uhandisi wa Ndege aliyoipata Tanzania na Canada, pamoja na Shahada za Diplomasia alizohitimu 2007 na 2021.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *