Serikali imesisitiza udhibiti wa matumizi sahihi ya fedha katika utekelezaji wa mradi wa afua za UKIMWI na Kifua Kikuu ngazi ya jamii baada ya mafanikio kuonekana katika awamu zilizopita.
Takwimu zinaonyesha maambukizi ya VVU yamepungua kwa asilimia 61, kutoka wagonjwa 110,000 mwaka 2010 hadi 43,000 mwaka 2024, huku wagonjwa wa Kifua Kikuu wakipungua kutoka 306 hadi 172 kwa kila watu 100,000.
Akizindua utekelezaji wa mzunguko wa saba wa mradi huo jijini Dar es Salaam, Katibu Mkuu Wizara ya Afya Dkt. Seif Shekalaghe amewataka watekelezaji, akiwemo Tume ya Kikristo ya Huduma za Kijamii (CSSC), kuhakikisha kila fedha inatumika kwa uadilifu na kufikia malengo yaliyopangwa.
✍ @claud_jm
#AzamTVUpdates