Umoja wa Mataifa umetahadharisha kuhusu hali mbaya ya kibinadamu nchini Sudan, ukieleza kuwa watu wengi katika eneo hilo wanahitaji msaada wa haraka.

Taarifa ya Umoja wa Mataifa imeeleza kuwa hali ya kibinadamu nchini Sudan inazidi kuzorota kwa kasi na kwamba takriban watu milioni 30 nchini humo wanahitaji msaada wa haraka.

Baada ya kuanguka kwa mji wa El Fasher, watu 90,000 wamekimbia makazi yao, na 50,000 katika jimbo la Kordofan wamelazimika kukimbia kutokana na kuongezeka kwa ghasia. Umoja wa Mataifa umesisitiza kuwa mgogoro wa Sudan unazidi kuwa mbaya na kwamba jamii ya kimataifa haipaswi kubakia katika hali ya kupuuza hilo.

Mapigano ya silaha nchini Sudan yalianza Aprili 15, 2023, kati ya jeshi linaloongozwa na Abdel Fattah al-Burhan na Vikosi vya Msaada wa Haraka vinavyoongozwa na Mohammed Hamdan Dagalo, kuhusu mamlaka na mvutano kuhusu jinsi Vikosi vya Msaada wa Haraka vinapaswa kujumuishwa katika jeshi baada ya mapinduzi ya 2021, na kufikia sasa upatanishi wa kimataifa haujazaa matunda.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *