Wazazi na walezi mkoani Dodoma wamehimizwa kuwapeleka shule watoto wanaotoka kwenye mkoa huo ili kukomesha dhana ya kuwa mkoa huo ndio tegemeo kwa kuzalisha wasaidizi wa kazi za ndani hususani wasichana wenye umri wa kwenda shule.
Katazo hilo limeenda sambamba na uwezeshwaji kwa watendaji mbalimbali wa Elimu wa jimbo la Mtumba ambalo Mbunge wake Anthony Mavunde ametoa vifaa mbalimbali zikiwemo mashine za kudurufu (Photocopier 20) kwa ajili ya kila kata sambamba na kompyuta mpakato 110 kwa ajili ya maafisa elimu, wakuu wa shule na walimu wakuu wa shule za msingi na sekondari jimboni humo.
Imeandaliwa na Ahmad Ally
Mhariri @moseskwindi