
Taarifa ya Ikulu ya kifalme imesema ziara hiyo inafanyika kwa mwaliko wa Rais wa Marekani na maelekezo ya Mfalme Salman. Mohammed atakutana na Rais Donald Trump kujadili uhusiano wa pande mbili na masuala ya maslahi ya pamoja. Ameongozana na mawaziri wa mambo ya nje, nishati na fedha. Mkutano wa ujumbe wake na Trump umepangwa kufanyika Jumanne hii katika Ikulu ya White House. Na taarifa ya Trump anasema mazungumzo hayo ni zaidi ya mkutano wa kawaida.