
Mashambulizi hayo ambayo yameharibu pia miundombinu kadhaa ya nishati, yamejiri wakati inaarifiwa kuwa utawala wa rais wa Marekani Donald Trump unaandaa kwa ushirikiano na Urusi , mpango wa amani ili kukomesha vita hivyo.
Hali hii imezusha pia maswali ya ikiwa rais Volodymyr Zelensky wa Ukraine atafanikiwa kuufufua mchakato wa amani katika ziara yake nchini Uturuki siku ya Jumatano na ambako anatarajiwa kukutana na mwenyeji wake Recep Tayyip Erdogan mjini Ankara ili kujadili namna ya kuumaliza mzozo huo.