Watu watano wamefariki dunia na mmoja kujeruhiwa katika ajali iliyotokea leo Novemba 23, 2025 maeneo ya Mbuyuni, Wilaya ya Monduli mkoani Arusha baada ya magari mawili kugongana.

Akithibitisha tukio hilo, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha, Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi, (SACP) Justine Masejo amesema ajali hiyo imetokea majira ya saa saba mchana na imehusisha basi aina ya Yutong lililokuwa likitokea Dodoma kuelekea Arusha na gari ndogo aina ya Mark X lililokuwa likitokea Arusha.

SACP Masejo ameeleza kuwa kati ya waliopoteza maisha, wanaume ni watatu na wanawake wawili, huku majeruhi akiwa ni mwanamke ambaye alikuwa miongoni mwa abiria waliokuwamo katika gari dogo.

Kwa mujibu wa Jeshi la Polisi, uchunguzi juu ya chanzo cha ajali hiyo unaendelea na majeruhi amelazwa katika Hospitali ya Jeshi Monduli kwa matibabu, huku miili ya marehemu ikihifadhiwa katika Kituo cha Afya Makuyuni.

#AzamTVUpdates

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *