#HABARI: Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP) ameondoa mashtaka dhidi ya mfanyabiashara wa vipodozi Jenifer Jovin (26), maarufu kama Niffer, pamoja na Mika Lucas Chavala, waliokuwa wakikabiliwa na kesi ya uhaini.
Uamuzi huo umetolewa leo, Desemba 3, 2025, mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu Aaron Lyamuya, baada ya Wakili wa Serikali, Titus Aron, kuiarifu Mahakama kuwa DPP hana nia ya kuendelea na shauri hilo dhidi ya washtakiwa.
Kwa hatua hiyo, Mahakama imewaachia huru rasmi washtakiwa hao waliokuwa wakishikiliwa kwa muda kwa tuhuma nzito zilizovuta hisia za watu wengi.
Powered by #MCHEZOSUPA
JINSI YA KUSHIRIKI MCHEZO SUPA:
–
Tuma 1000 kupitia Airtel Money, Tigo Pesa, M – Pesa, Halopesa, kwenda namba ya kampuni 222223 kumbukumbu namba ni 777 au weka neno ITV.
#ITVDigital #ITVUpdates #ITVTanzania
#Follow @itvtz @radioonetanzania
@capitaldigitaltanzania.