Dar es Salaam. Ebwanaeee wikiendi ndo imeanza hivyo. Kwa wale wapenzi wa muvi, tuwe tunakutana hapa kila Ijumaa kupeana vitu vitamu.

Hapa tutakuwa tukichambua kwa ufupi muvi ya wiki, kisha kukupa orodha ya mzigo wa kuburudika nao wikiendi nzima.

Pia tutakupa orodha ya kazi zinazotarajiwa kuachiwa ndani ya mwezi, ili mshkaji ujiandae kuzipokea kiroho safi na kuburudisha nafasi. Twende kazi…!

MUVI YA WIKI CARRY-ON

KIJANA mlinzi wa usalama Uwanja wa Ndege, Ethan Kopek, anajikuta msambweni katikati ya msimu wa sikukuu. Krismasi iko mlangoni, mkewe ni mjamzito na maisha yanaonekana kuwa ya kawaida kabisa. Kiu ya kutaka kukamata sasampa inambadilishia mazingira ya kazi ghafla kwa kupewa kazi ya kuwa mkaguzi wa mizigo.

Hata hivyo, mambo yanamchenjia ghafla pale anapokutana na abiria mtatanishi asiyemjua, anayeonekana kuwa na ombi lisilo la kawaida linalohusiana na mizigo yake inayopitia ukaguzi.

Hapo ndipo presha inaanza kupanda na kugeuza mchezo wa paka na panya unaokua taratibu katika kila hatua ya kazi yake na mwishowe kuwa na kibarua cha kuipambania familia yake na wakati huo huo kulinda kibarua chake.

Na hapo ndipo filamu hii inapozidi kunoga, kwani mtu aliyemweka mtegoni anabeba upande wa kitendawili kama mtu mwenye utulivu unaotia shaka, anayesababisha maswali mengi kuliko majibu na anayempelekesha Ethan kadri atakavyo kwa maelekezo maalumu yanayoishia kwao tu.

Hii ni moja ya filamu inayoweza kuteka hisia zako kwa muda wa dakika 110 na kama ni mpenzi wa thriller, usiikose kwani itakufanya uone muda ni kama unakimbia zaidi pale ukianza kuiangalia.

Muvi hii iliyotolewa mwaka 2024, imechezwa na Taron Egerton (Ethan Kopek), Jason Bateman (The Traveler), Sofia Carson (Nora Parisi), Danielle Deadwyler (Elena Cole), Tonatiuh Elizarraraz (Mateo Flores), Theo Rossi (The Watcher) na wengineo ikiwa imetayarishwa na Dylan Clark na kuongozwa na Jaume Collet-Serra, huku hadithi ikiandikwa na T.J. Fixman. Tukutane Ijumaa ijayo.

MZIGO WA WIKIENDI

Wikiendi ina mambo mengi na kama unataka kuifurahia wikiendi yako freshi ni vyema ukazitafuta hizi muvi tano ili usuuze roho yako!

1. Abigail

2. Dangerous Animals

3. Enemy at the Gates

4. Sleeping Dog

5. 12 Feet Deep

TANO ZIJAZO

Kama una mzuka mwingi wa kusubiri muvi mapya ndani ya Desemba, basi wala usikonde. Hapa kuna:

1. Man Finds Tape – Des 05

2. The Secret Agent – Des 05

3. Hunting Season – Des 05

4. The Chronology of Water – Des 05

5. Down River – Des 09

MKALI WA WIKI

Tom Cruise

Kuzaliwa: Julai 03, 1962

Mahali: Syracuse, New York

Fani: Mwigizaji na Mtayarishaji

Tangu: 1981 –

Kazi zake: Endless Love, Top Gun, Mission Imposible, Tha Last Samurai, Collateral, Knight & Day, The Mummy, Edge of Tomorrow, War of the Worlds, Magnolia, Far & Away, A Few Good Men.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *