
Karibu siku kumi baada ya mapinduzi nchini Guinea-Bissau mnamo Novemba 26, 2025, uongozi wa jeshii ilitangaza kuanzishwa kwa Baraza la Kitaifa la Mpito na hati ya mpito. Jeshi sasa limechukua udhibiti na kumteua mwendesha mashtaka mpya wa umma siku ya Ijumaa, Desemba 5.
Imechapishwa:
Dakika 1 Wakati wa kusoma
Matangazo ya kibiashara
Pamoja na mwandishi wetu maalum huko Bissau, Léa-Lisa Westerhoff
Ahmed Tidiane Balde, mkuu wa zamani wa Mahakama ya Wakaguzi, ambaye alikuwa na jukumu la kuthibitisha hesabu za umma, ameteuliwa kuwa mwendesha mashtaka wa umma na utawala wa kijeshi siku ya Ijumaa, Desemba 5, 2025. Kulingana na vyanzo kadhaa, yeye ni mshirika mwingine wa karibu wa rais aliyetimuliwa mamlakani Umaro Mokhtar Sissoco Embalo.
Nguvu za mwendesha mashtaka huyu zimeimarishwa na utawala wa kijeshi. Hili limeandikwa katika agizo Nambari 3, lililotolewa hadharani siku ya Alhamisi, Desemba 4, ambalo linatangaza kuanzishwa kwa hati ya mpito. Kifungu cha 1 cha agizo hili kinavunja Baraza Kuu la Mahakama. Hii inaashiria kutoweka kwa chombo hiki kinachohusika na kusimamia utawala wa sheria.
Mwendesha mashtaka wa umma, kwa upande wake, amepewa mamlaka makubwa. Anaweza kuteua naibu wake, kama Mwanasheria Mkuu, lakini pia kuteua majaji kuongoza mahakama mbalimbali nchini na kuamua uhamisho wao.
Kutoweka kwa usimamizi wa serikali
Chuo cha uongozi wa mahakama, ambacho huwafunza na kuwachagua majaji kupitia mitihani ya ushindani, kimesimamishwa kwa muda wote wa mpito. Kwa mwanachama wa chama cha kitaifa cha wanasheria, aliyewasiliana na RFI, amri hii inaashiria kutoweka kwa utawala wa sheria nchini Guinea-Bissau, kwani sasa hakuna chombo chochote cha kusimamia mamlaka ya utendaji inayoshikiliwa na jeshi.
Utawala wa kijeshi pia ulitangaza kuundwa kwa baraza la kitaifa la mpito. Uongozi wa jeshi bado haujatoa taarifa kuhusu idadi au utambulisho wa wanachama wake.
Baraza hili la mpito litatumika kuchukua nafasi ya Bunge la taifa, kwani mchakato mzima wa uchaguzi wa urais, pamoja na uchaguzi wa wabunge, ulisitishwa na mapinduzi wiki iliyopita.