
Katika taarifa iliyotolewa siku ya Alhamisi jioni, Desemba 4, Mwanasheria Mkuu wa Mahakama ya Rufaa ya Conakry alisisitiza kwamba mtu yeyote anayetambua utawala wa kijeshi na serikali kama wanaohusika na watu kutoweka na utekaji nyara atashtakiwa kwa kashfa na uchongezi.
Imechapishwa:
Dakika 1 Wakati wa kusoma
Matangazo ya kibiashara
Onyo hili kutoka kwa vyombo vya sheria vya Guinea linakuja katikati ya kampeni ya uchaguzi wa urais wa wa Desemba 28, 2025, ambapo Jenerali Mamadi Doumbouya ni mgombea. Hii inakuja huku idadi ya raia waliotoweka ikiendelea kuongezeka. Mfano wa hivi karibuni ni Massa Douago Guilavogui, mwanachama wa ofisi ya kisiasa ya chama cha upinzani cha Liberal Bloc.
Ni katika dakika za mwisho za matangazo ya habari za jioni ambapo Fallou Doumbouya, mwendesha mashtaka wa Mahakama ya Rufaa ya Conakry, alielezea hasira yake kuhusu kauli zinazosambazwa mara kwa mara kwenye majukwaa ya kidijitali ambazo kwa uwongo na kwa uchongezi zinahusisha utekaji nyara mkubwa na watu kutoweka kwa mamlaka ya umma: “Huu ni ukumbusho rasmi: kesi zote zilizoripotiwa za utekaji nyara au watu kutoweka zinahusiswa na kesi za kisheria za mara kwa mara mbele ya kitengo cha polisi wa mahakama, kwa mujibu wa masharti ya kifungu hicho.”
Idadi ya watu waliotoweka inaongezeka sana
Tangu utawala wa kijeshi wa CNRD wa Jenerali Mamadi Doumbouya ulipoingia madarakani, idadi ya watu wanaotoweka imeongezeka sana, hasa wanachama na wafuasi wa upinzani na mashirika ya kiraia. Katika baadhi ya matukio, mashahidi wengi wamewatambua wat waliovaa na kujihami kama vikosi vya usalama kama wahusika wa utekaji nyara huo. Mwendesha mashtaka aliongeza kuwa mashtaka haya sasa yatakabiliwa na vikwazo: “Kwa hivyo, mtu yeyote anayejaribu kuishutumu mamlaka ya umma kwa vitendo vya uhalifu atashtakiwa kwa kashfa, uchongezi, matusi, dharau, au kueneza habari za uwongo.”
Kulingana na Ofisi ya Kamishna Mkuu wa Haki za Binadamu wa Umoja wa Mataifa, angalau Waguinea kumi wanachukuliwa kuwa waathiriwa wa visa vya watu kutoweka kwa lazima. Visa vya hivi karibuni ni pamoja na naibu mkurugenzi wa kampeni wa mgombea Faya Millimono na jamaa wa msanii wa mtindo wa reggae Élie Kamano, wakiwemo watoto wake.