
Rais wa Senegal, Bassirou Diomaye Faye amesaini amri iliyozua gumzo nchini humo. Agizo hilo la rais lilitolewa siku ya Alhamisi, Desemba 4, linarekebisha ofisi ya Waziri Mkuu na kuimarisha mamlaka ya Waziri Mkuu. Lengo lililotajwa ni kuboresha “ufanisi” wa hatua za serikali. Kutolewa kwake kunakuja huku kukiwa na sintofahamu katika setrikali ambayo imeendelea kwa wiki kadhaa. Wengi wametoa hisia zao kutokana na agizo hilo la rais.
Imechapishwa:
Dakika 1 Wakati wa kusoma
Matangazo ya kibiashara
Na mwandishi wetu huko Dakar, Pauline Le Troquier
Katika vyombo vya habari nchini Senegal na kwenye mitandao ya kijamii, wengi wanabaini kwamba Ousmane Sonko anapata nguvu na nafasi ya kuingilia kati na agizo hili jipya la rais. Miongoni mwa wafuasi wa Pastef, baadhi hata wanaona kama ushindi kwa kiongozi wao katika mapambano ya madaraka na Bassirou Diomaye Faye, mapambano ya madaraka yaliyoanza mwezi mmoja mapema kuhusu ni nani anayepaswa kuongoza muungano wa “Diomaye Rais”.
Agizo hilo linalenga kupanua timu za Waziri Mkuu. Nafasi ya naibu mkurugenzi wa ofisi ya Waziri Mkuu na katibu wa serikali anayeshusika na masuala ya mahusiano na taasisi na msemaji wa serikali zimundwa. Washauri wa kiufundi pia wanaweza kuhamasishwa na mkuu wa serikali. Rasilimali nyingine anayoweza kutumia ni kitengo kilichojitolea mahsusi kwa ajili ya kuandaa mikutano ya Baraza la Mawaziri.
Kulingana na vyanzo kadhaa, huu ni upangaji upya wa kiutawala, suala rahisi la uwezo, ambalo halipanui mamlaka ya ofisi ya Waziri Mkuu kwa vyovyote vile. “Ni hatua ya kupunguza mvutano,” anabainisha mchanganuzi wa masuala ya siasa ambaye anabainisha kwamba rais anaonyesha nia ya kuendelea kufanya kazi pamoja na Ousmane Sonko, lakini “hajaacha hata chembe ya haki zake za kikatiba,” ameongeza.