Katika taarifa yake kwa vyombo vya habari mwakilishi huyo Maalum amelaani vikali jaribio hili la kutwaa madaraka kwa kutumia nguvu, ambalo amesema ni “ni tishio kubwa kwa uthabiti wa nchi hiyo na ukiukaji wa misingi ya msingi ya Katiba na utawala wa sheria.”

Anapongeza tangazo lililotolewa na mamlaka za Benin kwamba jaribio hilo la mapinduzi limezimwa na kwamba hali sasa imedhibitiwa, sambamba na kauli iliyotolewa na Waziri wa Mambo ya Ndani.

Wakati akieleza mshikamano wake na Serikali ya Benin, Rais Patrice Talon na wananchi wa Benin, Bw. Simão anahimiza mamlaka kuendelea na juhudi zao za kuhakikisha usalama wa wananchi na kurejesha hali ya utulivu kwa haraka na kikamilifu.

UNOWAS, kwa ushirikiano na washirika wake wa kikanda, itaendelea kuiunga mkono Benin katika juhudi zake za kuimarisha amani, demokrasia na uthabiti.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *