Vijana wa Kitanzania wamehimizwa kujiunga na vyuo vya usafiri wa anga vinavyotambuliwa na Shirika la Kimataifa la Usafiri wa Anga (ICAO) ili kupata utaalamu unaotambulika na kukubalika katika soko la ajira la dunia na kuongeza nafasi za kupata ajira.
Rai hiyo imetolewa na Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Ndege la Precision Air, Khalid Kaude wakati wa mahafali ya 15 ya mafunzo ya usalama wa ndani ya ndege yaliyotolewa na chuo kinachomilikiwa na shirika hilo.
Kwa upande wa wahitimu wa mafunzo hayo wameendelea kuyaomba mashirika ya ndege ya nchini na nje ya nchi kuongeza safari za ndani na nje ili kuongeza fursa kwa wasomi hao.
Mhariri @moseskwindi
(Feed generated with FetchRSS)