Baadhi ya mabasi ya masafa marefu mkoani Shinyanga yameripotiwa kuendesha safari kwa kuzidisha idadi ya abiria, kinyume na taratibu zilizowekwa na LATRA, hali inayochochea ongezeko la gharama kwa wasafiri katika msimu huu wa sikukuu za mwisho wa mwaka.

Uchunguzi wa waandishi wa habari ulibaini kuwa baadhi ya abiria walilazimika kulipia nauli zaidi ya kiwango kilichopangwa ili kupata nafasi ya kusafiri, huku wengine wakisafiri wakiwa katika mazingira yasiyo salama.

Hatua hiyo ilijitokeza wakati operesheni maalum ikiendeshwa chini ya Afisa Mfawidhi wa LATRA mkoani humo, Denis Magembe, kwa lengo la kubaini ukiukwaji wa taratibu za usafirishaji na kuwachukulia hatua kampuni na madereva waliokiuka sheria.

Mhariri | @claud_jm

#AzamTVUpdates #AdhuhuriLive #utv

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *