#HABARI: Mwenyekiti wa Chama cha wakristo wa Nigeria (CAN) katika Jimbo la Niger, Askofu Bulus Dauwa Yohanna, na Kamishna wa Polisi wa Jimbo la Niger, Adamu Abdullahi Elleman, wanasema wamepokea uthibitisho kwamba wanafunzi 100 waliotekwa kutoka Shule ya Kikatoliki ya St Mary huko Papiri wameokolewa na vikosi vya usalama.

Taarifa hiyo ilitoka katika Ofisi ya Mshauri wa masuala ya usalama wa Taifa, ambayo iliwafahamisha kwamba watoto hao wataachiliwa kwa makundi na kukabidhiwa kwa wazazi wao kuanzia Jumatatu.

Mshauri wa usalama wa Taifa, Nuhu Ribadu amefanya ziara Papiri wiki iliyopita na kukutana na ujumbe ulioongozwa na mmiliki wa shule hiyo, Askofu Yohanna, aliwahakikishia kwamba watoto hao wataokolewa hivi karibuni na kuungana tena na familia zao.

Jumla ya wanafunzi 165 bado hawajulikani walipo, huku wazazi wakisema wanasubiri kwa shauku taarifa kuhusu watoto wao.

Powered by #MCHEZOSUPA

JINSI YA KISHIRIKI MCHEZO SUPA:

📱Tuma 1000 kupitia Airtel Money, Tigo Pesa, M – Pesa, Halopesa, kwenda namba ya kampuni 222223 📱kumbukumbu namba ni 777 au weka neno ITV.

#ITVDigital #ITVUpdates #ITVTanzania
#Follow @itvtz @radioonetanzania
@capitaldigitaltanzania.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *