
Wakati wa kipindi maalum kwenye televisheni ya taifa jioni ya Jumapili, Desemba 7, Waziri wa serikali mpya ya Madagascar ametangaza kwamba mazungumzo haya yataandaliwa kwa pamoja na serikali na Baraza la Makanisa ya Kikristo. Mazungumzo hayo ambayo yatakadumu miezi sita, yatatoa nafasi kwa wadau wote katika jamii ya Madagascar na yatafikia kilele katika uandishi wa Katiba mpya.
Imechapishwa:
Dakika 1 Wakati wa kusoma
Matangazo ya kibiashara
Na mwandishi wetu huko Antananarivo, Guilhem Fabry
Karibu miezi miwili baada ya kupinduliwa kwa Andry Rajoelina nchini Madagascar, serikali ya Rais Michael Randrianirina, imeelezea taratibu za mashauriano ya kitaifa yajayo yatakayofanyika nchini humo. Wakati wa kipindi maalum kwenye televisheni ya kitaifa jioni ya Jumapili, Desemba 7, Waziri Hanitriniana Razafimanantsoa, kwanza aliahidi kwamba wadau wote kutoka jamii mbalimbali nchini humo watapewa nafasi ya kutoa maoni yao.
Alieleza kwamba raia wa Madagascar wangeweza kutoa wasiwasi wao na kupendekeza suluhisho katika ngazi ya fokonolona—jamii za watu kipato cha chini—kote kisiwani. Baadaye, utaratibu wa mashauriano katika ngazi za manispaa na kisha za kikanda ungeruhusu utashi wa wadau wote kutoka jamii mbalimbali: raia, viongozi wa kitamaduni, vyama, na wadau wa kisiasa na kiuchumi—kufikishwa hatua kwa hatua katika ngazi ya kitaifa.
Majadiliano hayo yatadumu kwa miezi sita. Hanitriniana Razafimanantsoa pia amebainisha kwamba mazungumzo haya yataanza kabla ya miezi mitatu, ili kutoa muda kwa vyombo vya dola kuanzisha mfumo ambao utafanyika. Mijadala hiyo itadumu kwa kipindi cha miezi sita na itaongozwa kwa pamoja na serikali na Baraza la Makanisa, mamlaka pekee halali ya kimaadili kuhakikisha uwazi, kutoegemea upande wowote, na ujumuishaji wa mchakato huo.
Hatimaye, Katiba mpya, ambayo itazaa Jamhuri ya Tano, itaandikwa mwishoni mwa mchakato huo, ifikapo mwezi Oktoba 2027, wakati kipindi cha mpito kitamalizika, Waziri Hanitriniana Razafimanantsoa ameeleza zaidi.