Mkoa wa Rukwa unapanga kutoa zaidi ya leseni 700 za uchimbaji na utafiti wa madini kwa wachimbaji wakubwa na wadogo, huku wawekezaji 10 tayari wakijitokeza kuonesha nia ya kuwekeza katika sekta hiyo baada ya kutangazwa kwa fursa hizo.

Afisa Madini wa Mkoa wa Rukwa, Mhandisi Joseph Mkumburu, alisema mpango huo unalenga kuongeza mapato ya ndani ya mkoa na kupanua wigo wa ajira, hususan kwa vijana, kupitia urasimishaji wa shughuli za uchimbaji.

Takwimu za ofisi ya madini zinaonesha kuwa utafiti wa awali umebaini uwepo wa zaidi ya hekta 3,000 zenye rasilimali za madini mbalimbali katika maeneo tofauti ya mkoa, hatua inayofungua uwezekano wa upanuzi wa shughuli za utafiti na uchimbaji katika wilaya kadhaa.

Mhariri | @claud_jm

#AzamTVUpdates #AdhuhuriLive

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *