
Mashambulizi hayo ya Alhamisi, Desemba 4, yanayohusishwa na Kikosi cha Msaada wa Haraka (RSF) cha Jenerali Hemedti, yanaripotiwa kusababisha vifo vya watu 79, wakiwemo watoto 40, kulingana na chanzo cha ndani kilichonukuliwa na shirika la habari la AFP. Mauaji haya ya hivi karibuni yanakuja wiki chache tu baada ya wanamgambo wa RSF kuteka mji wa El-Fasher, ambao pia wanashutumiwa kufanya ukatili huko.
Imechapishwa:
Dakika 2 Wakati wa kusoma
Matangazo ya kibiashara
Idadi ya vifo bado hajajulikani, lakini tayari inatarajiwa kuwa mbaya sana: nchini Sudan, mashambulizi ya ndege zisizo na rubani yaliwaua raia kadhaa, wakiwemo watoto wengi, siku ya Alhamisi, Desemba 4, huko Kalogi, mji unaodhibitiwa na jeshi la serikali katika jimbo la Kordofan Kusini, ambapo mapigano mengi kati ya jeshi na RSF ya Jenerali Hemedti kwa sasa yamejikita.
Baada ya kukamata El-Fasher, ngome ya mwisho ya jeshi huko Darfur, mwishoni mwa mwezi Oktoba, RSF ilihamisha mashambulizi yao katika eneo jirani, eneo la kilimo lenye rutuba ambalo pia lina utajiri wa dhahabu na mafuta.
Kulingana na afisa wa eneo hilo aliyenukuliwa na shirika la AFP, mji wa Kalogi lilishambuliwa mara tatu. Shambulio la kwanza linaripotiwa kulenga shule ya chekechea, la pili hospitali, huku la tatu likiwalenga “watu waliokuwa wanajaribu kuwaokoa watoto,” kulingana na Essam al-Din al-Sayed, mkuu wa kitengo cha utawala cha mji huo.
RSF yaonyooshewa kidole cha lawama
Kulingana na Essam al-Din al-Sayed, shambulio hilo—ambalo analihusisha RSF—liliwaua watu 79, wakiwemo watoto 40, idadi ambayo haiwezekani kuthibitishwa katika hatua hii kutokana na mawasiliano magumu katika eneo hili la mbali.
Mapema siku ya Alhamisi, Desemba 4, UNICEF ilithibitisha vifo vya zaidi ya watoto 10 wenye umri wa miaka mitano hadi saba. Kuhusu Umoja wa Afrika (AU), umeripoti vifo zaidi ya 100 katika taarifa iliyotolewa siku ya Jumapili, Desemba 7. Ingawa kukamatwa kwa El-Fasher na Vikosi vya Msaada wa Haraka (SFR) kulisababisha mauaji mengi, ubakaji, na uporaji, kulingana na ushuhuda mwingi kutoka kwa wanaharakati wa mashirika ya kibinadamu na manusura, Mwenyekiti wa Tume ya AU, Mahmoud Ali Youssouf, amesema kwamba “alishangazwa na ukatili unaoongezeka na unaorudiwa unaofanywa dhidi ya raia katika eneo hilo.”
Kufikia sasa, majaribio yote ya upatanishi yanayolenga kufikia usitishaji mapigano wa kweli nchini Sudan yameshindwa.