Waziri wa Ujenzi, Abdallah Ulega, amemsimamisha kazi Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA) ili kupisha uchunguzi wa tuhuma za uzembe, usimamizi dhaifu na ubadhirifu dhidi yake pamoja na baadhi ya viongozi wengine wa taasisi hiyo.
Ulega ametangaza uamuzi huo jijini Dar es Salaam kufuatia malalamiko kutoka kwa wananchi kuhusu utendaji wa TEMESA, pamoja na matokeo ya uchunguzi uliofanywa na tume maalum ya serikali.
Mhariri | John Mbalamwezi
#AzamTVUpdates