Rais Samia Suluhu Hassan ametuma salamu za rambirambi kwa Spika wa Bunge, Mussa Azzan ‘Zungu’ kufuatia kifo cha aliyekuwa mbunge wa Jimbo la Peramiho, Jenister Muhagama aliyefariki leo jijini Dodoma.
Katika salamu zake, Rais Samia amemuelezea kiongozi huyo kuwa alikuwa makini, mnyenyekevu, mchapakazi na mwenye historia ndefu ya kulitumikia katika nafasi mbalimbali za uongozi ndani ya Serikali na Bunge.
Aidha, Rais ametoa pole kwa wabunge, familia ya marehemu, ndugu na jamaa na wananchi wa Jimbo la Peramiho na kuwaombea moyo wa uvumilivu na subra katika kipindi hiki kigumu.
#StarTvUpdate