#HABARI: Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) leo imezindua rasmi jarida lenye tafiti mbalimbali zinazofanyika hospitalini hapo, na kuelezwa kuwa kila mwaka MNH hupokea maombi ya tafiti kati ya 400 hadi 500 zinazohusu maeneo tofauti ya huduma za afya, tiba na ustawi wa jamii.
Akizungumza wakati wa uzinduzi wa jarida hilo uliofanyika hospitalini hapo, Mkurugenzi Mtendaji wa MNH, Dkt. Delilah Kimambo, amesema Muhimbili ina jukumu muhimu katika kuboresha ubora wa huduma za afya nchini na kuimarisha sera za kitaifa kupitia tafiti hizo.
“Hatuwezi kuboresha huduma kama hatuna tafiti, zinatufanya tujue wapi tuweke kipaumbele. Jarida hili ni hatua muhimu ya kuonesha kazi kubwa inayofanywa na wataalam wetu katika kukuza ushahidi wa kitaalam,” amesema Dkt. Kimambo.
Aidha, ameongeza kuwa tafiti hizo husaidia kubaini changamoto za kiafya zinazoikabili jamii na kuweka misingi ya kuboresha huduma kwa kutumia ushahidi. Pia zinachangia kujenga uwezo wa kitaaluma kwa wafanyakazi wa afya nchini kupitia ushiriki wao katika kufanya na kuchambua tafiti hizo.
Powered by #MCHEZOSUPA
JINSI YA KUSHIRIKI MCHEZO SUPA:
–
📱Tuma 1000 kupitia Airtel Money, Tigo Pesa, M – Pesa, Halopesa, kwenda namba ya kampuni 222223 📱kumbukumbu namba ni 777 au weka neno ITV.
#ITVDigital #ITVUpdates #ITVTanzania
#Follow @itvtz @radioonetanzania
@capitaldigitaltanzania.