#HABARI: Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Njombe (CHAUMMA), Bi. Sigrada Mligo, amelalamikia Serikali uwepo wa utitiri wa tozo mbalimbali kwa wafanyabiashara wa mazao ya misitu jambo ambalo limekuwa kisababishi cha rushwa kwa mamlaka zinazohusika.
Bi. Sigrada ametoa malalamiko hayo wakati akizungumzia mambo mbalimbali juu ya maendeleo ya Mkoa wa Njombe, katika kikao kazi cha Mkuu wa Mkoa wa Njombe Anthony Mtaka pamoja na Madiwani, CMT na viongozi wote wa taasisi na sekta binafsi za Mkoa huo.
Katika hatua nyingine, Bi. Sigrada ametoa wito kwa Serikali kuongeza watendaji wa Mahakama akiwemo Hakimu wa Mahakama ya Ardhi, ili kupunguza vifo vya Wananchi kwa kukosa haki kutokana na kesi zitokanazo na migogoro ya ardhi kukaa muda mrefu Mahakamani.
“Mkoa mzima wa Njombe tuna Hakimu mmoja wa Mahakama ya Ardhi ambaye anazunguka wilaya zote kwa hiyo kesi nyingi, zinacheleweshwa. Inafika mahali Mzee amehangaika na kesi miaka 10 na watu wanakufa kwa ‘stress’, kesi haiishi kila siku yeye ni kuhudhuria Mahakamani,” amesema Sigrada.
Aidha, Sigrada amesema kuna kila sababu pia ya kurekebisha mfumo ili kila Wilaya iweze kuwa na Mwenyekiti wa Baraza Wilaya ambaye atakuwa Hakimu, ili kupunguza kucheleweshwa kwa kesi hususani za ardhi ambazo zipo kwa kiasi kikubwa mkoani Njombe.
Powered by #MCHEZOSUPA
JINSI YA KUSHIRIKI MCHEZO SUPA:
–
📱Tuma 1000 kupitia Airtel Money, Tigo Pesa, M – Pesa, Halopesa, kwenda namba ya kampuni 222223 📱kumbukumbu namba ni 777 au weka neno ITV.
#ITVDigital #ITVUpdates #ITVTanzania
#Follow @itvtz @radioonetanzania
@capitaldigitaltanzania.