“Kingine ambacho ningependa Serikali ifanye ni kuwekeza Kimataifa kwenye Media za kwao ambazo wanazimiliki. Mfano leo hii watu wanazungumzia TBC wana TBC Sports.
“Na TBC ni Shirika la Utangazaji la Serikali kwa hiyo Serikali ina uwezo wa kutengeneza mchango wake katika kukuza tasnia ya habari Kimataifa wakiamua kuwekeza zaidi kwenye media yao na wakifanya iwe kubwa Kimataifa.
“Leo hii tunataka habari ili dunia itujue kuhusu sisi Watanzania, Serikali kama ikiamua kuwekeza sana kwenye media yake Kimataifa dunia nzima ikawa inasema source ya habari labda ni Shirika la Utangazaji la Tanzania (TBC).
“Ile itawatangaza kama nchi na pia vijana wetu watakuwa wakifanya kazi kama waandishi watakuwa na uwezo wa kuitangaza na kwenda kwenye sehemu kubwa duniani kama ambavyo TBC wanapeleka waandishi kwenye michuano mikubwa ya dunia.
“Serikali iwekeze kwenye media yao ya ndani iwepo mfano TBC International kwa ajili ya kuitangaza Tanzania Duniani. Na kuwasaidia waandishi kwenda kwenye platform kubwa za Kimataifa”- @JohnJackson_jj
#LiveonClouds360
#LainiYaWana
#Clouds26Nyoosha