Shirika la Reli Nchini (TRC) linatarajia kuanza ujenzi wa reli ya kisasa katika maeneo mbalimbali ya Dar es Salaam, ikiwa ni hatua muhimu ya kutatua changamoto ya usafiri na foleni katika jiji hilo.
Akizungumza mara baada ya ziara ya kukagua hali ya utoaji huduma wa shirika hilo katika kituo cha treni ya kisasa ya SGR cha Magufuli, Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Albert Chalamila, pamoja na Mkurugenzi wa TRC, Mhandisi Machibya Shiwa wamesema ujenzi wa reli hiyo utaanza 2026.
#AzamTVUpdates
Mhariri | John Mbalamwezi