#HABARI: Mkurugenzi wa Huduma za Uhandisi wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA) Mha. Erick Madinda, amesema kuwa TPA inatekeleza jumla ya miradi 16 ya kimkakati, yenye umuhimu mkubwa kwa uchumi wa taifa, ambapo thamani yake inakadiriwa kufikia zaidi ya shilingi trilioni 8.2.

Akizungumza kuhusu utekelezaji wa miradi hiyo, Mha. Madinda amesema miradi hiyo imepewa kipaumbele kutokana na mchango wake katika kuimarisha huduma za kibandari, kupunguza changamoto za usafirishaji, na kuongeza uwezo wa Serikali kukusanya mapato kupitia shughuli za bandari.

Pia amesema huduma za kibandari nchini zina mchango mkubwa katika mapato ya Serikali, kupitia shughuli za kibandari na hivyo TPA imejipanga kuhakikisha miundombinu yote inayohitajika inakamilika kwa wakati ili kuongeza ufanisi wa bandari zake.

Kati ya miradi 16 ya kimkakati, miradi tisa tayari inaendelea kutekelezwa katika maeneo mbalimbali. Mojawapo ya miradi hiyo ni ujenzi wa Bandari Mpya ya Mbamba Bay, ambayo inalenga kufungua rasmi ukanda wa kusini (Southern Corridor).

Amesema kuwa eneo la Mbamba Bay lina fursa kubwa hasa baada ya nia na mipango ya Serikali kujenga reli kutoka Mtwara hadi Mbamba Bay ambayo itaongeza kwa kiasi kikubwa uunganishaji wa miundombinu ya majini na nchi kavu.

Kwa sasa, bandari ya Mbamba Bay ilikuwa na uwezo mdogo na haikidhi mahitaji ya kisasa, hivyo TPA imeanza ujenzi wa bandari mpya kabisa ambapo bandari ya zamani itabaki pembeni huku ujenzi wa miundombinu ya kisasa ukiendelea.

Mha. Madinda alisisitiza kuwa kukamilika kwa miradi hii kutaiwezesha Tanzania kuongeza ushindani katika sekta ya usafirishaji, kupunguza gharama za uendeshaji, na kuongeza mapato ya Serikali kupitia bandari zinazoendelea kujengwa na kuboreshwa.

Powered by #MCHEZOSUPA

JINSI YA KUSHIRIKI MCHEZO SUPA:

Tuma 1000 kupitia Airtel Money, Tigo Pesa, M – Pesa, Halopesa, kwenda namba ya kampuni 222223 kumbukumbu namba ni 777 au weka neno ITV.

#ITVDigital #ITVUpdates #ITVTanzania
#Follow @itvtz @radioonetanzania
@capitaldigitaltanzania

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *