#HABARI: Rais wa Rwanda Paul Kagame, amesema hahusiki na ukiukwaji wa makubaliano yaliyosainiwa baina yake, Marekani na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo wiki iliyopita mjini Washington.
Rais Kagame amesisitiza kwamba mapigano Mashariki mwa Kongo yamekuwa yakiendelea hata kabla ya mapatano hayo kutiwa saini.
Kongo na nchi za Magharibi wamekuwa wakiishtumu Rwanda kwa kuunga mkono waasi wa M23, waliouteka mji wa Uvira katika Kivu ya kusini mapema wiki hii mara tu baada ya makubaliano hayo kusainiwa.
Akizungumza katika hafla ya kuapisha baadhi ya viongozi walioteluliwa Serikalini, Rais Paul Kagame amesema yeye binafsi amekuwa chini ya shinikizo kubwa hasa na tuhuma zinazoihusisha Rwanda katika vita vinavyoendelea Mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.
Alisema kuwa mkataba kati ya Rwanda, DRC na Marekani ulitiwa saini mjini Washington mnamo Desemba 4, 2025 nchi yake ilishiriki kwa hiari na kwa nia ya amani huku akisema Rwanda imeukubali na itatii matakwa yake ili makubaliano hayo yaweze kuongoza nchi hizo mbili kwa amani.
Powered by #MCHEZOSUPA
JINSI YA KUSHIRIKI MCHEZO SUPA:
–
Tuma 1000 kupitia Airtel Money, Tigo Pesa, M – Pesa, Halopesa, kwenda namba ya kampuni 222223 kumbukumbu namba ni 777 au weka neno ITV.
#ITVDigital #ITVUpdates #ITVTanzania
#Follow @itvtz @radioonetanzania
@capitaldigitaltanzania.