Idadi ya nchi zilizosusia mashindano ya Eurovision zikipinga kushirikishwa utawala wa Kizayuni katika mashindano hayo, imeongezeka.
Katika hatua ya karibuni kabisa, Shirika la Utangazaji la Redio na Televisheni la Iceland limetangaza kuwa halitashiriki kwenye mashindano ya muziki ya Eurovision 2026. Sababu iliyotangazwa na shirika hilo la Iceland ya kujitoa katika mashindano hayo na kupinga kushiriki Israel kwenye mashindano ya Eurovison 2026.
Ireland, Uhispania, Uholanzi na Slovenia zimesusia michuano hiyo baada ya utawala wa Kizayuni kukubaliwa kushiriki katika mashindano ya muziki ya Eurovision 2026.
Mashindano ya Wimbo la Eurovison yaani (Eurovision Song Contest) ni moja ya matukio makubwa zaidi ya muziki duniani ambayo yamekuwa yakiendeshwa kila mwaka na Jumuiya ya Utangazaji ya Ulaya tangu mwaka 1956. Mashindano hayo yalianzishwa kwa lengo la kujenga mshikamano wa kitamaduni kati ya nchi za Ulaya, lakini baada ya muda kupita, yamekuwa ni sherehe ya muziki duniani ambapo hata nchi za nje ya Ulaya kama Australia, pia hushiriki katika mashindano hayo. Umuhimu wa Eurovision hauishii tu katika kipengele chake cha burudani. Mashindano hayo ni jukwaa la kudhihirisha utamaduni, lugha na utambulisho wa miziki ya nchi mbalimbali.
Kuongezeka idadi ya nchi ambazo zimeamua kususia Mashidano ya Wimbo la Eurovision kwa ajili ya kupinga kushiriki utawala wa Kizayuni kwenye mashindano hayo kunatajwa kuwa ni moja ya matukio muhimu sana ya kiutamaduni na kisiasa barani Ulaya kuwahi kushuhudiwa katika miaka ya hivi karibuni. Hatua hiyo si tu imeathiri nyanja za kisanii na burudani za hafla hiyo, lakini pia limekuwa ni jukwaa la kubainisha wazi upinzani wa kisiasa na kimaadili. Sababu za ususiaji huu na taathira zake zinaweza kuchunguzwa katika maeneo kadhaa.
Sababu ya kwanza ya kususiwa, ni mgogoro wa kibinadamu huko Gaza na kuuliwa shahidi makumi ya maelfu ya raia wa Palestina. Nchi na vyombo vingi vya umma vinaamini kuwa kushiriki Israel katika mashindano hayo ya Eurovision kunamaanisha kupuuza maadili ya kibinadamu na thamani za dunia. Kwa mfano, vyombo vya habari vya kitaifa huko Ireland, Uhispania, Uholanzi na Slovenia vimetangaza kuwa litakuwa jambo lisiloweza kuhalalishwa kuendelea kushiriki kwenye mashindano hayo katika hali ambayo Israel imetenda jinai za kivita na kukiuka haki za binadamu na imeruhusiwa kushiriki kwenye mashindano hayo. Nchi hizo zimesisitiza kuwa thamani kama uhuru wa vyombo vya habari, utu wa binadamu na haki ya kuishi havipasi kuwa mhanga wa sera za Jumuiya ya Utangazaji ya Ulaya.

Sababu ya pili inahusiana na tuhuma kwamba Israel imeingilia moja kwa moja mchakato wa kupiga kura na utangazaji wa Mashindano ya Wimbo wa Eurovision. Ripoti zilizotolewa zinaonesha kuwa taasisi za serikali za utawala wa Kizayuni zimejaribu kubadilisha matokeo ya kura za umma katika mchuano huo kwa manufaa yake kupitia kuendesha propaganda maalumu na kampeni za vyombo vya habari. Suala hili limedhoofisha imani ya nchi nyingi zilizokuwa zinaamini kwamba mashindao hayo hayapendelei upande wowote na kupelekea baadhi ya vyombo vya habari kutangaza kwamba havina tena imani na mchakato wa uendashi wa mashindano ya Eurovision.
Kwa kweli kuongezeka nchi zilizosusia Eurovision zikilalamikia kushiriki utawala wa kizyauni katika mashindao hayo kumeakisi uhusiano mkubwa uliopo kati ya utamaduni na siasa. Ususiaji huu si tu umetilia shaka uhalali wa mashindano hayo, bali pia umekuwa ni silaha ya mashinikizo ya kisiasa na kimaadili dhidi ya utawala wa Kizayuni. Ikiwa hali hiyo itaendelea, Eurovision itabadilika kutoka tamasha la muziki la Ulaya na kuwa jukwaa la mijadala ya kisiasa na maadili kati ya makundi mawili ya nchi zinazounga mkono na zinazopinga Uzayuni barani Ulaya, na bila ya shaka mustakabali wake utaathiriwa pakubwa.