Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), Dkt. Delilah Kimambo, amesema tafiti zinazofanyika katika hospitali hiyo ni nyenzo muhimu katika kuleta mageuzi ya huduma za afya nchini kwa kuboresha ubora wa huduma na kuongeza ujuzi wa wataalamu.
Akizungumza wakati wa uzinduzi wa jarida la tafiti la Muhimbili, Dkt. Kimambo amesema tafiti hizo husaidia kufuatilia mwenendo wa magonjwa na mabadiliko ya vimelea.
#AzamTVUpdates
✍ Upendo Micheal
Mhariri | John Mbalamwezi