Brigedia Jenerali Ali Jahanshahi,  Kamanda wa vikosi vya nchi kavu vya Jeshi la Jamhuri ya Kiislamu ya Iran vikosi vya ulinzi vikiwa na zana kamili, silaha na uwezo viko tayari kukabiliana na tishio lolote la adui kwa kusikiliza amri ya Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu.

Akisisitiza mamlaka na utayarifu kamili wa vikosi vya jeshi amesema: “Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, kwa kutegemea uwezo wa ndani, mwongozo wa busara wa Kiongozi Muadhamu na uungaji mkono wa wananchi, ilimzuia adui kufikia malengo yake maovu katika vita vya kutwishwa vya siku 12 mwezi Juuni mwaka huu.

Kamanda wa Jeshi la Nchi Kavu la Iran amesema, kutokana na Iran kuwa katika eneo maalum la kijiografia, mipaka mirefu, na kupakana na majirani nyingi, inachukuliwa kuwa moja ya maeneo ya kijiografia ya ulimwengu na Asia Magharibi, na imekuwa ikitishiwa na maadui katika historia. Jahanshahi aliongeza: “Nguvu yoyote ambayo itadhibiti Mlango-Bahari wa Hormuz inashikilia nishati na uchumi wa dunia mikononi mwake.”

Amesema: “Leo majeshi ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran yana mambo makubwa ya kusema katika uga wa teknolojia mpya, na uwezo huo ni matokeo ya kuamini uwezo wa ndani.

Brigedia Jenerali Jahanshahi amesema, Marekani imejaribu kuudhoofisha mfumo wa Kiislamu na kuusambaratisha kwa kutumia zana na njama mbalimbali vikiwemo vikwazo vya kidhalimu lakini imeshindwa katika njia hiyo. Aliongeza: “Maadui walijaribu hata kugawanya nchi, lakini mradi huu pia mara zote umeshindwa na kugonga mwamba.”

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *