Mwili wa aliyekuwa Mbunge wa Peramiho wawasili Abasia ya Mtakatifu Benedikto Peramiho, misa ya kumuombea yafanyika

Mwili wa aliyekuwa Mbunge wa Jimbo la Peramiho, Mhe. Jenista Mhagama, umewasili katika Kanisa Katoliki la Abasia ya Mtakatifu Benedikto Peramiho kwa ajili ya ibada maalum ya misa ya kumuombea marehemu, huku waombolezaji wengi wakijitokeza kushiriki katika tukio hilo la kihistoria na lenye huzuni kubwa.

Misa hiyo imehudhuriwa na viongozi mbalimbali wa Kitaifa akiwemo Dkt. Mwigulu Nchemba, Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Musa Zungu, pamoja na Spika Mstaafu wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Tuli Akson. Viongozi hao, pamoja na waumini na wananchi, wameungana katika sala na dua kumuombea marehemu pamoja na kuifariji familia yake.

#CloudsDigitaUpdates

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *