Ukaguzi uliofanywa na kikosi cha usalama barabarani mkoani Geita umebaini kuwa kuelekea mwisho wa mwaka kuna ongezeko la tabia hatarishi miongoni mwa baadhi ya madereva wanaofanya shughuli zao kwa kuangalia maslahi binafsi bila kuzingatia usalama wa abiria.
Akizungumza katika stendi kuu ya mabasi Geita, Afisa Mnadhimu wa Kikosi cha Usalama Barabarani nchini, SACP Butusyo Mwambelo, amesema miongoni mwa changamoto zilizobainishwa ni pamoja na matumizi ya pombe kwa baadhi ya madereva wakati wa safari kwa madai ya kuzuia usingizi, pamoja na kufanya safari za mara kwa mara bila kupumzika, hali inayochangia ajali nyingi zinazotokana na makosa ya kibinadamu.
Unashauri nini kifanyike kupunguza wimbi la ajali za barabarani kuelekea mwisho wa mwaka
#AzamTVUpdates