#HABARI: Mwili wa aliyekuwa Mbunge wa Peramiho, Jenista Mhagama unatarajiwa kuzikwa leo katika Makaburi ya Senta B yaliyopo Kijiji cha Ruanda, Halmashauri ya Mbinga mkoani Ruvuma, karibu na kaburi la mumewe, marehemu Leonard Mhagama ambaye alifariki mwaka 2010.
Mwili wa marehemu umewasili katika Kijiji cha Ruanda tayari kwa ibada fupi ya misa, kabla ya kupelekwa rasmi katika makaburi hayo kwa ajili ya maziko.
Mazishi hayo yanahudhuriwa na viongozi mbalimbali pamoja na waombolezaji kutoka maeneo tofauti, ambapo Makamu wa Rais, Dkt. Emmanuel Mchimbi anatarajiwa kuwaongoza waombolezaji.
Powered by #MCHEZOSUPA
JINSI YA KUSHIRIKI MCHEZO SUPA:
–
Tuma 1000 kupitia Airtel Money, Tigo Pesa, M – Pesa, Halopesa, kwenda namba ya kampuni 222223 kumbukumbu namba ni 777 au weka neno ITV.
#ITVDigital #ITVUpdates #ITVTanzania
#Follow @itvtz @radioonetanzania
@capitaldigitaltanzania