Serikali imemtaka mkandarasi anayejenga daraja la Ilambo, wilayani Sumbawanga, mkoani Rukwa kuanza ujenzi huo mara tu baada ya Sikukuu ya Zawadi “Boxing Day” na kukamilisha ujenzi huo ndani ya miezi sita aliyoahidi.

Kauli ya Serikali imetolewa na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu – Kazi, Ajira na Mahusiano, Deus Sangu na kuongeza kuwa fedha za ujenzi huo takribani milioni 900 zimeshaidhinishwa.

#AzamTVUpdates
Mhariri | @moseskwindi

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *