Watu wenye ulemavu wilayani Mbulu wameiomba Serikali kuwapa kipaumbele kwenye kupata mikopo ya asilimia 10 inayotolewa na halmashauri ili kuwawezesha kufanya shughuli mbalimbali za kuwainua kiuchumi.
Katika utaratibu huo, asilimia mbili ya mikopo hiyo ni maalum kwa ajili ya watu wenye ulemavu.
Mikopo hiyo imelenga kuimarisha shughuli zinazowaingizia kipato wanawake, vijana na watu wenye ulemavu wasio na ajira rasmi.
#AzamTVUpdates
✍ Hellen Kawiche
Mhariri | @claud_jm