Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, George Simbachawene ameitahadharisha jamii ya Watanzania kujiepusha na msukumo wa dhulma, uongo na ubinafsi unaoenezwa kupitia mitandao ya kijamii akisema umekuwa ukiongezeka kutokana na matumizi ya teknolojia.
Waziri Simbachawene ametoa rai hiyo leo, Disemba 25, 2025 wakati wa ibada ya Krismasi iliyosaliwa katika kanisa la Parokia ya Pwaga, wilayani Mpwapwa, mkoani Dodoma.
#AzamTVUpdates
Mhariri | @moseskwindi