Mamlaka ya Mapato nchini (TRA) imepongeza ulipaji kodi wa hiyari sambamba na sera za uchumi kuwa kiini cha muendelezo wa mafanikio ya kuvuka malengo la ukusanyaji wa kodi huku mamlaka hiyo ikikusanya Shilingi Trilioni 9 na Bilion 800 katika robo ya pili ya mwaka 2025 ambayo ni zaidi ya Shilingi Bilioni 140 ya lengo la kukusanya Trilioni 9 na Bilioni 660.
#AzamTVUpdates
Mhariri | @moseskwindi