Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Russia amekosoa vikali vitisho vya Marekani na utawala wa Kizayuni dhidi ya Iran, na kusema jamii ya kimataifa inapinga sera hizo za vitisho.

Kwa mujibu wa Pars Today, Maria Zakharova, msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Russia, Jumanne usiku alitoa onyo dhidi ya kurudia makosa mabaya ya Juni 2025, akiashiria vita vya siku 12 vya utawala wa Kizayuni na Marekani dhidi ya Iran. Amesisitiza kuwa Moscow inawaonya ‘tawhidi wa misimamo mikali’ kujiepusha na kuchochea mvutano na Iran na mpango wake wa nyuklia, na badala yake waachane na njia yao ya uharibifu.

Moscow inawaonya ‘wenye  misimamo mikali’ kujiepusha na kuchochea mvutano na Iran na mpango wake wa nyuklia, na waachane na njia yao ya uharibifu.

Zakharova alionyesha wasiwasi mkubwa kuhusu kauli za Benjamin Netanyahu, Waziri Mkuu wa utawala wa Kizayuni, tarehe 29 Disemba wakati wa ziara yake Marekani, kuhusu uwezekano wa mashambulizi ya kijeshi dhidi ya Iran, ikiwemo miundombinu yake ya nyuklia. Amesema vitisho hivyo vinapingana na sheria za kimataifa na Hati ya Umoja wa Mataifa, vinadhoofisha mfumo wa kutokomeza uenezaji wa silaha za nyuklia, na vinaweza kusababisha maafa ya kinyuklia na kibinadamu katika eneo. Zakharova amesisitiza haja ya kufikia makubaliano ya kidiplomasia yanayoheshimu mikataba na kuzingatia maslahi halali ya Iran.

Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Russia amesisitiza kuwa juhudi za kueneza mtazamo kwa jamii ya kimataifa kwamba suala la mpango wa nyuklia wa Iran linaweza kutatuliwa kwa kutumia nguvu za kijeshi na mashambulizi, ikiwemo dhidi ya vituo vilivyo chini ya usimamizi na uangalizi wa Shirika la Kimataifa la Nguvu za Atomiki (IAEA), hazikubaliki kabisa.”

Kwa mujibu wa Zakharova, mitazamo isiyo na uwajibikaji kama hiyo inauharibu mfumo wa kimataifa wa kuzuia uenezaji wa silaha za nyuklia, ambao Mkataba wa Kuzuia Uenezaji wa Silaha za Nyuklia (NPT) ndio msingi wake. Amesema haiwezekani kupuuzia ukweli kwamba vitisho hivi vinatolewa na upande ambao si mwanachama wa mkataba huo, ilhali Iran ni mwanachama na mara kwa mara imethibitisha utii wake kwa wajibu wa kisheria.

Ameongeza kuwa mzigo wa kiitikadi wa kupinga Iran katika kauli kama hizi si jambo jipya. Aidha, jamii ya kimataifa mara nyingi imekataa mitazamo ya aina hiyo, kwa kuwa misimamo hiyo inapingana na kanuni za sheria za kimataifa na Katiba ya Umoja wa Mataifa, na inaweza kulitia eneo la Asia ya Magharibi katika hatari ya madhara makubwa ya kibinadamu na ya kinyuklia.

Ameongeza kuwa mzigo wa kiitikadi wa kupinga Iran katika kauli kama hizi si jambo jipya. Aidha, jamii ya kimataifa mara nyingi imekataa mitazamo ya aina hiyo, kwa kuwa misimamo hiyo inapingana na kanuni za sheria za kimataifa na Katiba ya Umoja wa Mataifa, na inaweza kulitia eneo la Asia ya Magharibi katika hatari ya madhara na maafa makubwa ya kibinadamu na ya kinyuklia.

Msimamo thabiti wa Russia  katika kukataa vitisho vipya vya Marekani na utawala wa Kizayuni unaonyesha mtazamo wa Moscow wa kupinga hatua zisizo halali za Washington na Tel Aviv dhidi ya Iran, hususan baada ya kurejea kwa Donald Trump madarakani kama Rais wa Marekani mnamo Januari 2025.

Bango linaloashiria namna Trump na Netanyahu wanavyochukiwa kutokana na sera zao za kivita

Hatua ya Russia kukemea vitisho vya Marekani na utawala wa Kizayuni dhidi ya Iran  kunapaswa kuchambuliwa katika muktadha wa mabadiliko ya kijiografia ya kisiasa ya eneo na mashindano ya kimataifa. Hatua hii si msimamo wa kidiplomasia wa kawaida tu, bali inabeba ujumbe mzito na wenye nukta kadhaa kwa Washington na Tel Aviv. Kupitia msimamo huu, Russia inaonyesha dhamira ya kuchukua nafasi yenye nguvu zaidi katika mahesabu ya kiusalama  Asia ya Magharibi na kulinda maslahi yake mbele ya mashinikizo ya Magharibi.

Sababu ya kwanza ya kukemea vitisho hivyo inapaswa kutazamwa katika uhusiano mpana kati ya Moscow na Tehran. Iran ni mshirika muhimu kwa Russia katika eneo, iwe katika sekta ya nishati au katika masuala ya kiusalama. Ushirikiano wa nchi hizi mbili nchini Syria, pamoja na katika nyanja za kiuchumi na kijeshi, umeonyesha kuwa Moscow haitaki kuiacha Tehran peke yake. Kukemea vitisho vya Marekani na utawala wa Kizayuni, kwa hakika, ni ishara ya msaada wa kisiasa kwa Iran na kuimarisha ushirikiano huu wa kimkakati.

Sababu ya pili inahusiana na ushindani wa Russia  na Marekani. Katika miaka ya hivi karibuni, Moscow imejitahidi kusimama dhidi ya siasa za upande mmoja za Washington. Kukemea vitisho dhidi ya Iran ni fursa kwa Russia kuonyesha kuwa inapinga mashinikizo ya Marekani si tu barani Ulaya bali pia katika Asia ya Magharibi. Hatua hii ni ujumbe wa wazi kwa Washington kwamba Russia iko tayari kukabiliana na siasa za kuingilia mambo ya ndani ya Marekani katika kila kona ya dunia.

Kwa upande mwingine, Russia kupitia msimamo huu inatoa onyo kwa utawala wa Kizayuni wa Israel. Tel Aviv katika miaka ya hivi karibuni imeitishia Iran mara kadhaa, na hatimaye kwa kushirikiana na Marekani mnamo Juni 2025 ilianzisha vita vya kichokozi dhidi ya Iran. Hivyo Russia kuikemea Israel ni jambo linalodhihirisha kuwa Moscow inaona vitendo na vitisho hivyo kama vinavyovuruga uthabiti wa eneo, na haitakubali kukaa kimya. 

Sababu nyingine inapaswa kutazamwa katika juhudi za Russia za kuthibitisha nafasi yake kama nguvu huru ya kimataifa. Moscow kupitia msimamo huu inataka kuonyesha kuwa katika hesabu za kimataifa si mfuasi wa Magharibi pekee, bali inaweza kusimama pamoja na mataifa huru yanayopinga utawala wa mabavu. Hatua hii pia ni ishara kwa fikra za umma duniani, hususan katika nchi zinazoendelea, kwamba Urusi inaunga mkono kanuni ya mamlaka ya kitaifa na inapinga vitisho na mashinikizo ya kigeni.

Kwa jumla, msimamo wa Russia wa kukosoa na kukemea vitisho vya Marekani na utawala wa Kizayuni dhidi ya Iran  kunapaswa kutazamwa kama hatua yenye sura nyingi: inatoa maana kwa ushirikiano wa kimkakati na Tehran, inaimarisha ushindani na Washington, na pia ni ujumbe wa tahadhari kwa Tel Aviv. Msimamo huu unaonyesha jitihada za Russia za kuchukua nafasi yenye nguvu zaidi katika Asia ya Magharibi na kuthibitisha nafasi yake kama nguvu huru ya kimataifa.”

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *