Aliyekuwa rais wa Madagascar aliyeondolewa mamlakani, Andry Rajoelina, amezungumza kwa mara ya kwanza tangu alipopinduliwa kama rais wa Madagascar katikati ya mwezi Oktoba. “Kutokana na vitisho, mivutano, na mgawanyiko, ni kwa dhamiri njema kwamba nimechagua kujiuzulu,” amesema.

Imechapishwa:

Dakika 1 Wakati wa kusoma

Matangazo ya kibiashara

Rais wa zamani wa Madagascar, Andry Rajoelina, amechagua kuzungumza kwa mara ya kwanza katika ujumbe ulioelekezwa kwa raia wa Madagascar ajili ya Mwaka Mpya. Karibu miezi mitatu baada ya kutimuliwa kwake madarakani, ametoa ujumbe wa amani na kuelezea sababu ya ukimya wake katika maandishi yaliyochapishwa kwenye ukurasa wake wa Facebook.

Picha kwenye kadi yake ya salamu ya mtandaoni mwanzoni inaonyesha utulivu: akiwa amevaa nguo nyeupe, akiwa amezungukwa na njiwa na matawi ya mizeituni, Andry Rajoelina anaonekana akiwa na tabasamu na sura ya utulivu.

“Nchi yetu, Madagascar, inapitia kipindi kigumu.” Katika maandishi yanayoambatana, mkuu wa zamani wa nchi anatoa ujumbe wake wa amani, ujasiri, na matumaini, kisha anazungumzia mgogoro unaokabili Kisiwa hiki: “Nchi yetu, Madagascar, inapitia kipindi kigumu, mtihani unaoonyeshwa na wasiwasi, kutokuwa na uhakika, na wakati mwingine hofu. Kwa wale ambao wako katika mazingira magumu na wanaoteseka, wale ambao wanahisi kuteswa, mnajua kwamba hamko peke yenu.” 

Zaidi ya yote, Andry Rajoelina amezungumzia sababu za ukimya wake: “Kutokana na vitisho, mivutano, na mgawanyiko ambao tumepitia, ni kwa dhamiri njema kwamba nilichagua kujiuzulu, badala ya kuwavuta raia wa Madagascar katika mapambano na machafuko.”

Kisha alikataa pendekezo lolote la kulipiza kisasi na hatimaye akataka umoja na uwajibikaji.

Kanali Randrianirina, 51, aliapishwa kama “Rais wa Ufufuo” mnamo Oktoba 17, siku chache baada ya kikosi chake, Capsat, kujiunga na harakati ya maandamano ya kiraia iliyoanza mwezi mmoja mapema. Rais Andry Rajoelina na wasidizi wake walitoroka kisiwa hicho kwa msaada wa Ufaransa.

Mwanajeshi mpya wa Madagascar, Kanali Michael Randrianirina, alielezea nia yake, katika mahojiano na kituo cha televisheni cha France 24, kwamba Andry Rajoelina, aliyelazimika kukimbia mwezi Oktoba, ahukumiwe nchini Madagascar.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *