#HABARI: Naibu Waziri wa Afya, Dkt. Florence Samizi, kwa niaba ya Waziri wa Afya Mhe. Mohamed Mchengerwa, ametembelea na kuwajulia hali majeruhi wa ajali ya basi na lori iliyotokea usiku wa Disemba 31, 2025 katika kijiji cha Maseyu, mkoani Morogoro.
Akizungumza wakati wa ziara hiyo, Dkt. Samizi amesema majeruhi 5 wanaendelea kupatiwa matibabu katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Morogoro, majeruhi 2 wamepewa rufaa kwenda Taasisi ya mifupa Muhimbili kwa matibabu zaidi, huku majeruhi 16 wakiruhusiwa kurejea majumbani baada ya hali zao kuimarika.
Aidha, kuhusu marehemu, amesema kuwa miili 4 tayari imetambuliwa, ambapo miili 3 imekabidhiwa kwa ndugu kwa ajili ya mazishi. Ameongeza kuwa miili 6 ilichukuliwa vinasaba (DNA) kwa ajili ya utambuzi, na kati ya hiyo mwili 1 tayari umetambuliwa, huku ndugu wakisubiri kukamilika kwa taratibu za Kipolisi ili kuuchukua. Kwa sasa, miili 5 inaendelea kusubiri majibu ya vinasaba.
Naibu Waziri ametoa wito kwa ndugu na jamaa wa marehemu ambao bado hawajatambulika kufika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Morogoro kwa ajili ya kusaidia zoezi la utambuzi wa miili na kukamilisha taratibu za mazishi.
Powered by #MCHEZOSUPA
JINSI YA KUSHIRIKI MCHEZO SUPA:
–
Tuma 1000 kupitia Airtel Money, Tigo Pesa, M – Pesa, Halopesa, kwenda namba ya kampuni 222223 kumbukumbu namba ni 777 au weka neno ITV.
#ITVDigital #ITVUpdates #ITVTanzania
Follow @itvtz @radioonetanzania
@capitaldigitaltanzania.