Zaidi ya asilimia 25 ya wananchi waliojitokeza kupata huduma za uchunguzi wa afya katika kambi maalumu iliyoendeshwa na Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI) kwa kushirikiana na Arusha Lutheran Medical Center, wamegundulika kuwa na shinikizo la juu la damu.
Akizungumza kuhusu matokeo ya uchunguzi huo, Mkurugenzi Mtendaji wa JKCI, Dkt. Peter Kisenge, amesema kuwa takribani asilimia tano ya wagonjwa hao tayari wameanza kupata madhara kwenye misuli ya moyo, hali iliyosababisha moyo kutanuka kutokana na presha ya damu isiyotibiwa ipasavyo.
Dkt. Kisenge amesisitiza umuhimu wa uchunguzi wa mapema na ufuatiliaji wa matibabu ili kuzuia madhara makubwa ya magonjwa ya moyo.
✍Ramadhani Mvungi
#AzamTVUpdates