Hisia zimekuwa nyingi tangu operesheni ya kijeshi ya Marekani iliyosababisha mashambulizi dhidi ya Caracas na kutekwa nyara kwa Nicolas Maduro na mkewe. Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres anasema ni hatari na kwamba sheria ya kimataifa haijaheshimiwa. Umoja wa Ulaya (EU) umetoa wito wa kuheshimiwa kwa sheria ya kimataifa na kusisitiza kujitolea kwake kwa mpito wa kidemokrasia na amani nchini Venezuela. Barani Afrika, pia, wengi wametoa hisia zao.

Imechapishwa:

Dakika 1 Wakati wa kusoma

Matangazo ya kibiashara

Kwanza, Umoja wa Afrika (AU). Shirika hilo limechagua maneno yake kwa uangalifu. Halijalaani moja kwa moja hatua ya kijeshi ya Marekani nchini Venezuela, bali ukumbusho dhahiri wa kanuni. Umoja wa Afrika unabainisha tena kujitolea kwake kwa sheria ya kimataifa, heshima kwa uhuru wa nchi, uadilifu wao wa eneo, na haki ya watu kujitawala. Umoja wa Afrika pia umesisitiza umuhimu wa mazungumzo, utatuzi wa migogoro kwa amani, na kutoa wito kwa pande zote kujizuia.

Afrika Kusini yatoa msimamo wake

Kwa upande wa nchi za Afrika, Afrika Kusini imetoa msimamo wake. Pretoria inazungumzia ukiukaji wa wazi wa Mkataba wa Umoja wa Mataifa. Inakumbusha kwamba sheria ya kimataifa hairuhusu uingiliaji kati wa kijeshi kutoka nje katika masuala ya ndani ya taifa huru. Afrika Kusini inatoa wito kwa Baraza la Usalama kukutana haraka pamoja na Caracas.

Kwa upande wake, Waziri wa Mambo ya Nje wa Venezuela Ivan Gilles anasema kwamba amefanya majadiliano mengi na viongozi wa Afrika. Anataja jumbe za mshikamano, hasa kutoka Namibia, Burkina Faso, na Liberia, ambazo Waziri wake wa Mambo ya Nje anahakikisha kwamba nchi yake, ambayo si mwanachama wa kudumu wa Baraza la Usalama, itadai hatua na kulaani mashambulizi ya Januari 3.

Hakuna nchi inayounga mkono uingiliaji kati wa nchi za kigeni ka nchi huru

Caracas pia inasema imezungumza na mawaziri wa mambo ya nje wa Chad, Angola, Niger, na Gambia. Wote, kulingana na Venezuela, wamejitolea kuheshimu Mkataba wa Umoja wa Mataifa na kufutilia mbali uingiliaji wowote wa mataifa ya kigeni kuingiliwa katika nchi iliyo huru na ambayo inajitawala.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *