Balozi na mwakilishi wa kudumu wa Somalia katika Umoja wa Mataifa amesema kuwa, hatua ya Israel ya   ya kulitambua rasmi eneo la ‘Somaliland’, ambalo limejitenga na Somalia, kama taifa huru na lenye mamlaka kamili kuwa ni njama kupotosha maoni ya umma kutokana na uhalifu unaoendelea kufanywa na utawala huo katika Ukanda wa Gaza.

Abukar Dahir Osman, mwakilishi wa kudumu wa Somalia katika Umoja wa Mataifaamesema hayo katika kikao cha Baraza la Usalama na kueleza kwamba, Somalia haitakubali kamwe na malengo ya utawala huu ya kuwahamisha Wapalestina milioni moja na nusu kutoka Gaza hadi Somaliland.

Somaliland ilijitenga na Somalia mwaka 1991 kufuatia vita vikali vya wenyewe kwa wenyewe lakini haijawahi kutambuliwa rasmi na nchi yoyote mwanachama wa Umoja wa Mataifa. Jamhuri hiyo iliyotangaza kujitenga na Somalia imeanzisha sarafu yake, bendera na bunge, ingawa maeneo yake ya mashariki yameathiriwa na mzozo.

Mogadishu imepinga madai hayo ya kuwa taifa huru Somaliland na kusema kuwa eneo hilo ni sehemu ya Somalia.

Akizungumzia kulaaniwa kimataifa hatua ya Israel ya kuitambua rasmi Somaliland, Rais Sheikh Mahmoud wa Somalia amesema: “Utawala wa Kizayuni umechukua hatua hiyo tulipokuwa tumekaribia kutatua matatizo ya muda mrefu ya nchi yetu na kujaribu kuunganisha nchi kwa amani.”

Mataifa na asasi mbalimbali za Kiafrika, Kiarabu na Kiislamu zimepinga vikali hatua ya utawala vamizi wa Israel ya kulitambua rasmi eneo la ‘Somaliland’, ambalo limejitenga na Somalia, kama taifa huru na lenye mamlaka kamili, hatua ambayo imekabiliwa na radiamali kali ya Jumuiya ya Nchi za Kiarabu na jamii ya kimataifa.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *