‎#HABARI: Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete, amempongeza Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kulinda tunu ya amani na mshikamano wa taifa, huku akiwahimiza Watanzania kuongeza maombi ili changamoto zilizojitokeza mwaka 2025 zisijirudie tena.

‎Dkt. Kikwete ametoa kauli hiyo wakati wa uzinduzi wa Jengo la Afisi ya Uhamiaji na Makazi ya Askari lililopo Wilaya ya Micheweni, Mkoa wa Kaskazini Pemba, ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya miaka 62 ya Mapinduzi ya Zanzibar.

‎Katika tukio hilo, Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhe. George Simbachawene, na Kamishna Jenerali wa Uhamiaji, Dkt. Anna Makakala, wameahidi kuendelea kuboresha mazingira ya kazi kwa askari na kusogeza huduma za Uhamiaji karibu zaidi na wananchi.

‎Powered by #MCHEZOSUPA


‎JINSI YA KUSHIRIKI MCHEZO SUPA:
‎-
‎Tuma 1000 kupitia Airtel Money, Tigo Pesa, M – Pesa, Halopesa, kwenda namba ya kampuni 222223 kumbukumbu namba ni 777 au weka neno ITV.

‎#ITVDigital #ITVUpdates #ITVTanzania
‎#Follow @itvtz @radioonetanzania
‎@capitaldigitaltanzania.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *