Mamlaka ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi (VETA), inatarajia kujenga vyuo 65 zaidi ili kutoa fursa kwa Vlvijana wengi nchini kupata elimu ya ufundi.
Akizungumza katika
Maonesho ya Kimataifa ya Biashara Zanizbar (ZITF) yanayoendelea katika viwanja vya Dimani Meneja wa kapuni Tanzu ya VETA (Ujuzi Incoparated Company Limited), Marco Kapinga amesema mpaka sasa VETA ina jumla ya vyuo 80 hapa nchini na vyuo 65 viko katika hatua ya ujenzi ambako 64 ni vya ngazi ya wilaya na kimoja ni kinajengwa kwa ngazi ya mkoa (Songwe).
Kwa mujibu wa meneja huyo, kukamilika kwa ujenzi huo kutafanya mamlaka hayo kufikisha vyuo 145 Tanzania bara.
Kapinga amewakaribisha wananchi wa Zanzibar kufika katika banda la VETA ili kushuhudia bidhaa zinazopatikana lakini pia kupata taarifa za mafunzo ya ufundi stadi na fursa zake.
Meneja huyo amesema kampuni imenza na kazi takribani 23 ambako ipo katika mfumo wa manunuzi wa Serikali (NesT), ikifanya biashara ya kuuza bidhaa zinazotokana na mbao ikiwamo samani za ofisini, hoteli, shule na nyumbani.
#StarTvUpdate