#HABARI: Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Balozi Dkt. Bashiru Kakurwa, amewaagiza wasimamizi wa mradi wa soko la Kimataifa la dagaa maarufu kama Chato Beach, kuhakikisha vizimba vya soko hilo vinatolewa kwa walengwa waliokusudiwa wakati wa kuanzishwa kwa mradi huo.
Balozi Dkt. Bashiru ametoa maagizo hayo mara baada ya kukagua hatua za ujenzi wa mradi huo na kuelekeza kuwa uanze kutumika mara tu utakapo kabidhiwa rasmi na mkandarasi ifikapo Februari 28, 2026.
Pia Dkt. Bashiru ameagiza wataalam wa Wizara kushirikiana na wale wa Halmashauri ya Wilaya ya Chato kupanga utaratibu wa kumpata mwendeshaji wa soko hilo pamoja na mtambo wa kuhifadhi ubora wa dagaa kupitia teknolojia ya ukaushaji.
Mradi wa Chato Beach unatarajiwa kuwa kitovu cha biashara ya Kimataifa ya dagaa na kuongeza thamani ya mazao ya uvuvi nchini.
Powered by #MCHEZOSUPA
JINSI YA KUSHIRIKI MCHEZO SUPA:
-
Tuma 1000 kupitia Airtel Money, Tigo Pesa, M – Pesa, Halopesa, kwenda namba ya kampuni 222223 kumbukumbu namba ni 777 au weka neno ITV.
#ITVDigital #ITVUpdates #ITVTanzania
#Follow @itvtz @radioonetanzania
@capitaldigitaltanzania.