#HABARI: Waziri wa Nishati wa Tanzania, Mhe. Deogratius Ndejembi, amebainisha kuwa mradi wa bomba la mafuta ghafi (EACOP) umefungua fursa kubwa za kiuchumi, ikiwemo ajira takribani 12,000.
Katika ajira hizo, Watanzania wamenufaika na nafasi 8,500 huku Waganda wakipata nafasi 3,500, hali inayochochea biashara za ndani na maendeleo ya kijamii katika maeneo yanayopitiwa na mradi huo kuanzia Uganda hadi jijini Tanga.
Mradi huu wa kimkakati, unaomilikiwa na kampuni za TotalEnergies, TPDC, UNOC na CNOOC, unahusisha ujenzi wa bomba lenye urefu wa kilomita 1,443 lenye uwezo wa kusafirisha mapipa 246,000 ya mafuta kwa siku. Kwa sasa, ujenzi umefikia asilimia 79, ukiambatana na miundombinu ya kisasa kama matangi manne makubwa ya kuhifadhi mafuta na gati la baharini lenye urefu wa kilomita mbili huko Chongoleani, Tanga.
Utekelezaji wa mradi unatarajiwa kukamilika ifikapo Julai 2026, huku shehena ya kwanza ya mafuta ikitarajiwa kusafirishwa mwezi Oktoba 2026. Mawaziri wa nchi zote mbili wamepongeza ushirikiano wa Marais Dkt. Samia Suluhu Hassan na Yoweri Museveni, huku wakisisitiza matumizi ya nishati safi kama jua katika kuendesha mradi huo ili kupunguza uzalishaji wa hewa ukaa.
Powered by #MCHEZOSUPA
JINSI YA KUSHIRIKI MCHEZO SUPA:
–
Tuma 1000 kupitia Airtel Money, Tigo Pesa, M – Pesa, Halopesa, kwenda namba ya kampuni 222223 kumbukumbu namba ni 777 au weka neno ITV.
#ITVDigital #ITVUpdates #ITVTanzania
#Follow @itvtz @radioonetanzania
@capitaldigitaltanzania.